Waheshimiwa na madiwani wa kiongozwa na Mwanyekiti wa Halmashauri ya Lushoto pamoja na Timu ya wakuu wa Idara wakiongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri wakiwa kwenye mafunzo maalum ya maadili ya viongozi na watumishi wa umma kutoka kwa mkufunzi kutoka sekretariati ya maadili ya viungozi na watumishi wa umma kutoka kanda ya Mashariki. Katika mafunzo hayo mada mbili ziliwasilishwa ikiwamo mgogano wa maslai na utaratibu mzuri wa kujaza fomu za maadili za viongozi wa umma wakiwemo wah. Madiwani.Katika mada ya Mgongano wa Maslai viongozi wamesisitizwa kutofanya biashara na tasisi inayoifanyia kazi, Kutotumia rasmali za taasisi kwa manufaa binafsi, kujiuzulu kwenye nafasi au kwenye vikao vyenye maamuzi ambayo yanaweza kumnafaisha kiongozi husika, Kutopokea zawadi ambazo zinaweza kutoa upendeleo kwa mtu aliyetoa hiyo zawadi na kutotengeneza mazingira ya kupewa rushwa.
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa