- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Lushoto Mh. Methew Mbaruku na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Bi. Ikupa Harrison Mwasyoge. Leo Tarehe 21/01/2022 wamekabidhi Pikipiki Mbili kwa Maafisa Ugani wawili wa Kata mbili za Halmashauri ya wilaya ya Lushoto. Maafisa Ugani waliokabidhiwa pikipiki ni Saidi Bakari ambaye ni Afisa Ugni wa Kata ya Shume na Omary Mahimbo Afisa ugani wa Kata ya Lushoto.
Zoezi hilo la Kukabidhi pikipiki kwa Maafisa ugani lilifanyika Mbele ya Jengo la Halmashauri ya wilaya ya Lushoto na kushuhudiwa na Watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.
Mh. Methew Mbaruku aliwaambia Maafisa ugani hao watumie pikipiki hizo kwa matumizi mazuri ya kiofisi ambayo yataleta maendeleo kwa Umma na kukuza kipato.
Pia Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Lushoto, Bi. Ikupa Harrison Mwasyoge aliwambia maafisa ugani hao wawe waangalifu katika mwendo ambao wanautumia kuendesha pikipiki hizo na kuwashauri waendeshe kwa mwenda wa kawaida ili kuhepusha ajali kwao na kwa wengine.
Pikipiki hizo ambazo zimegawiwa kwa maafisa ugani katika halmashauri zote nchini.
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa