- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
Mkuu wa Mkoa wa Tanga ndg. Martin Shigella aongoza mkutano wa baraza maalum la hoja za mwaka wa fedha 2017/2018 katika Halmashuri ya Lushoto na kushiriki zoezi maalum la kutoa mikopo yenye thamani ya sh.33,500,000/= wanawake vijana na watu wenye ulemavu.Katika Mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Lushoto ndg .Ikupa Mwasyoge alitoa taarifa ya kuwepo hoja takribani hamsini ambazo ziliibuliwa na Mkaguzi mkuu wa serikali na kutolewa majibu .Kaimu mkaguzi wa ndani aliwasilisha taarifa hiyo kwa niaba ya mweka hazina wa Halmashauri na kuwapitisha waheshimiwa madiwani majibu yote ya manajimenti kisha madiwani wa katoa maoni yao. Katika Mkutano huo wah. Madiwani walielezwa kuwa katika ukaguzi uliofanyika kwa kipindi cha kuishia tarehe 30 juni 2018 Halmashauri ya wilaya ya Lushoto ilipata HATI SAFI.Mkuu wa Mkoa wakati anahitimisha mkutano huo alitoa pongezi kwa managementi nzima ya Halmashauri kwa kazi nzuri iliyofanyika na kuhakisha Halmashuri inapata hati safi tofauti na mwaka uliopita. Alisisitiza jitihada hizo ziendelee na mwaka huo wa fedha na kuhakisha hoja za mkuguzi wa ndani zinafanyiwa kazi mapema na kutolewa majibu kwa wakati,pia na kuahidi kuwa anatuma wataalam wakupitia vitabu vya hoja kabla ya kupelekwa kwa CAG kuhakikisha majibu yanajibiwa vizuri
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa