- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
Mwenge wa uhuru umewasili mkoani Tanga ukitokea mkoa wa kilimanjaro tayari kwa kuanza mbio zake katika Halmashauri zote za Mkoa wa Tanga kwa kuanzia Halmashauri za ya Lushoto na Bumbili.Mwenge huo ulipokelewa mpakani mwa mkoa Tanga na Kilimanjaro katika kijiji cha mkomazi na Mkuu wa Mkao wa Tanga Mh.Martin Shegella akiongazana na Kamati za ulinzi na usalama za mikoa na wilaya pamoja na viongozi mbalimbali wa chama na serikali katika mkoa humo wakiwemo wabunge wa lushoto bumbuli na mlalo wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri zote na wakuu wa idara na vitengo.
Katika Halmashauri ya Lushoto mwenge ulipitia miradi mbalimbali na kuzindua mradi wa kiwanda cha kuchakata zao la mkonge, Kufungu maabara ya sayansi katika shule ya Kwemaramba na kufungua club ya kuzuia rushwa shuleni hapo, pia mwenge ulitembelea mradi wa kuotesha miti ya kupanda kwa ajili ya kutunza mazingira na kutoa cheti wa "friends of Usambara" . Mwenge wa uhuru alfajiri ya tarehe 4/10/2018 uliendelea na mbio zake katika halmashauri ya Bumbuli na kuhitimisha mbio zaka katika wilaya ya Lushoto tarehe 5/10/2018 na kukabidhiwa katika Wilaya ya Korogwe.
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa