- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
Suleimani Mzee Suleimani katibu wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Tanga akiwa na baadhi Wajumbe wa CCM mkoa wa Tanga wafanya ziara ya siku mbili tarehe 01-02/02/2022 kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo. Wakiwa katika Wilaya ya Lushoto waliongozana na viongozi Mbalimbali wa Wilaya. Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Mh Karist Lazaro. Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Lushoto, Mh Methew Mbaruku. Wah. Madiwani Kutoka Kata mbalimbali za Wilaya ya Lushoto. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Lushoto, Bi. Ikupa Harrison Mwasyoge na Wakuu wa Idara mbalimbali wa Halmashauri ya wilaya ya Lushoto.
Ziara hiyo ilitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo kata mbalimbali za Wilaya ya Lushoto. Baadhi ya Miradi iliyotembelewa ni Mradi wa Kituo cha Afya Mtae. Ujenzi wa Vyumba viwili vya madarasa , matundu sita ya choo na Ofisi ya walimu katika shule ya Msingi Mpanga. Miradi yote ya ujenzi shule ya Sekondari Shambalai. Ujenzi katika shule ya Sekondari Nywelo na Kwenda Kutembelea Shule ya watoto wenye mahitaji maalumu ya Irente.
Katika ziara hiyo. Katibu wa Chama cha mapinduzi (CCM), Suleimani Mzee Suleimani aliwatembelea mabarozi wa Mashina.
Pia aliongea na wananchi kwa kuwahimizi kujikinga na kuchukua Tahadhari zote za Ugonjwa wa Uviko-19 na Ugonjwa wa Ukimwi
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa