- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
Sekta
|
Aina ya mradi wa uwekezaji
|
Maelezo ya mradi
|
Mapendekezo ya mfumo wa uwekezaji
|
Eneo lililopo na mahali lililpo
|
Mazingira rafiki yanayoruhusu uwekezaji
|
|
Ujenzi wa mashine ya kisasa kwa ajili ya kukoborea mpunga –Mng’aro
|
Uwekezaji huu unahitajika sana kwa sababu kwa sasa wakulima wanauza mpunga badala ya mchele na hii ni kwa sababu hakuna mashine nzuri za kukoboa mpunga. Kwa mfano uzalishaji kwenye skimu hii umeongezeka kutoka tani 3 kwa hecta mwaka 2008 hadi tani 5.5 mwaka 2010 kutokana na mafunzo waliyopatiwa wakulima kati ya mwaka 2008/2009 hadi 2011/2012. Uzalishaji umeongezeka lakini hakuna soko la uhakika kwa sababu mazao hayajaongezewa thamani kitu kinachowavunja moyo sana wakulima.
|
Ubia kati ya serikali na wananchi
|
Wilaya ya Lushoto ina skimu nne maarufu kwa kilimo cha Umwagiliaji yaliyopo kwenye kijiji cha Mng’aro, Lunguza, Kivingo na Kwemkwazu, vijiji hivi vipo kwenye kata ya Mng’aro, Lunguza na Mnazi ambazo zipo tarafa ya Umba iliyopo kwenye ukanda wa tambarare upande wa Kaskazini mwa Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga. Skimu hizi zipo kati ya 70 to 100 km kutoka Lushoto mjini na zimpakana na Hifadhi ya taifa ya Mkomazi.
|
Serikali/Halmashauri imetoa eneo kwa ajili ya shughuli za uwekezaji
|
Kuanzisha kituo cha mashine za Kilimo
|
Shughuli nyingi kwenye hii skimu ikiwa ni pamoja na maandalizi ya shamba, uchakataji wa mbegu, uvunanji na usafirishaji unafanywa kwa mikono kitu kinachofanya ufanisi kuwa mdogo sana, Hivyo kama uwekezaji wa mashine mbalimbali kama trekta, jembe la kukokotwa na ng’ombe, mashine ya kupandia mpunga, mashine za kusafirishia na za kuvunia utafanyika kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali zitaazimwa na kufanya kazi hizo. Hii itapelekea kuongeza eneo la uzalishaji, kuotesha kwa wakati na kuongeza ufanisi katika kilimo kwenye skimu hii ya Mng’aro.
|
Ubia kati ya muwekezaji,wananchi na Halmashauri.
|
Eneo hili lipo katika nyuzi 9498050N - 9501400N, 430450E – 437600 Mashariki na muinuko wa mita 400 toka usawa wa bahari na linafikika kwa mwaka mzima.
|
Serikali/Halmashauri imeridhia uwekezaji kufanyika katika eneo hili.
|
|
Uwekezaji kwenye maduka ya pembe jeo za kilimo. (Mng’aro na Lunguza)
|
Fursa iliyopendekezwa kwa maeneo ya Mng’aro na Lunguza ni uanzishaji wa Maduka ya pembejeo za kilimo.Serikali inatoa mbolea na mbegu za ruzuku kwa wakulima katika skimu hii lakini hazi wafikii wakulima wote. Hivyo basi uanzishwaji wa maduka haya utawezesha wakulima kupata pembe jeo hizi kwa wakati kwa kutumia vocha hivyo kuongeza uzalishaji.
|
Ubia kati ya muwekezaji serikali na wananchi
|
Eno lenye uhitaji wa huduma hii yanafikika kwa mwaka mzima suala ambalo limuahakikishia muwekezaji
|
Wakulima wako tayari kutoa ushirikiano endapo huduma hiyo itapatikana sambamba na mahitaji yao.
|
|
Kutanua eneo la kilimo na Kuanzisha kilimo cha Mkataba–Lunguza na Mng’aro
|
Eneo linalolimwa ni 1,530ha kati ya eneo la zaidi ya 3,030ha. linalofaa kawa kilimo.Kama atapatikana mwekezaji anayetumia mashine na ujuzi wa kisasa atakayelima eneo linalofaa kwa kilimo na ambalo halilimwi husuani Lunguza ambapo eneo kubwa linalofaa kulima halijalimwa, uzalishaji utaongezeka zaidi ya mara mbili kwani eneo lililolomwa ni karibu ya nusu ya eneo linafaa kwa kilimo cha umwagiliaji.
|
Ubia kati ya muwekezaji na wananchi
|
Kwa mwaka eneo hili linapata kati ya 600mm–750mm za mvua. Hali ya joto ni kati ya 25oC and 30oC na hali ya unyevu wa 70%. Skimu ipo kati ya Longitudo 9498050N - 9501400N na Latitudo 430450E - 437600E pia lipo 400m juu kutoka usawa wa bahari.
|
Wakulima wako tayari kutoa ushirikiano endapo huduma hiyo mikiwepo.
|
|
Eneo hili linapendekezwa kwa uwekeaji wa viwanda vya kusindika MALINDI -KILUWASHA
|
Uhitaji wa kuongeza thamani mazao ya mbogamboga ni mkubwa na hivyo umuhimu wa kujenga kiwanda kidogo cha usindikaji unaonekana. Idadi kubwa ya wakulima watakuwa na uhakika wa upatikanaji wa soko la bidhaa zitakazozalishwa na kuongezwa thamani.Eneo hili linamilikiwa na serikali ya kijiji cha Malindi ambao ndio waliohakikishia kuwa tayari kumkaribisha mwekezaji kwa ajili ya kulitumia eneo hili lenye umeme wa
|
Ubia kati ya muwekezaji na wananchi
|
Eneo hili linafika kwa mwaka mzima kupitia uwepo wa barabara ya changarawe kutoka Lushoto mjini mpaka Malindi kwa umbali wa kilometa 70 -100 na muinuko wa mita 1622 kutoka usawa wa bahari.
|
Serikali ya kijiji kupitia ridhaa ya wananchi imeridhia uwekezaji kufanyika katika eneo hili.
|
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa