- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
IDARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO.
Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ni mojawapo ya idara za Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto. Idara hii inaratibu utekelezaji wa shughuli mbalimbali zikiwemo uwezeshaji wa wananchi kiuchumi, maendeleo ya watoto, usajili na uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, ushirikishwaji jamii, maendeleo ya jinsia na masuala mtambuka kama mazingira, rushwa, UKIMWI, Afya ya jamii, Bima ya Afya, jinsia na lishe.
Maeneo ya kiutawala
Idara ya Maendeleo ya Jamii, jinsia, wazee na watoto ina jumla ya madawati matano ya utekelezaji ambayo ni Dawati la uwezeshaji wa wananchi kiuchumi na kupunguza umaskini (dawati linashughulika na kusimamia Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake, Vijana na Walemavu); Dawati la Ushirikishwaji jamii linaloratibu Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF; kuwezesha jamii kupanga na kutekeleza shughuli za maendeleo; kutambua fursa na vikwazo vya maendeleo ya jamii na namna ya kushirikisha jamii kushiriki kwenye shughuli za maendeleo; na kutoa elimu kwa jamii kuhusu miradi mikubwa ya kimkakati kama umeme na barabara inayotekelezwa na serik ali; Dawati la uratibu wa maendeleo ya jinsia; Dawati la uratibu wa maendeleo ya mtoto, Dawati la usajili na uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs); na Dawati la uratibu wa masuala mtambuka (Utunzaji wa Mazingira, Jinsia, Mapambano dhidi ya Rushwa, Mapambano dhidi ya UKIMWI, Afya ya Jamii, Bima ya Afya na Lishe).
Malengo ya Idara
Kuwezesha jamii boresha ustawi wa hali ya maisha, kupata haki na kupata huduma bora za kijamii na kiuchumi kwa kushirikishwa na kushiriki katika kupanga, kuamua, kutekeleza, kusimamia na kutathimi shughuli za maendeleo.
Majukumu ya Idara
Idara ya Maendeleo ya Jamii, jinsia, wazee na watoto inatekeleza majukumu yafuatayo:
Mafanikio ya Idara
Idara imefanikiwa kufikia ufanisi mkubwa kwenye utekelezaji wa majukumu yake. Mathalani, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kuanzia 2015/2016 hadi 2019/2020, idara imetekeleza majukumu yafuatayo kwa mafanikio makubwa kama ifuatavyo:
Changamoto za Idara
Idara inakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazochangia kushindwa kutekeleza shughuli zake kama zilivyopangwa. Changamoto hizo ni kama zifuatazo:
Dira
Idara kuwa kinara katika kutoa huduma kwa uwazi kufikia matokeo ya kijamii na kiuchumi kwa maendeleo endelevu ifikapo 2025.
Dhamira
Idara kutoa huduma bora za kiuchumi na kijamii kwa uwazi kwa kutumia vizuri rasilimali zilizopo kuboresha ustawi wa jamii ili kufikia maendeleo endelevu.
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa