- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
HALMASHAURI ya Wilaya ya Lushoto imewatunuku vyeti vya pongezi Watendaji Kata, Maafisa Ugani pamoja na Waganga Viongozi waliofanya vizuri Katika ukusanyaji wa mapato kwa Mwaka wa Fedha 2024 - 2025 na Kuweka mikakati ya kuboresha ukusanyaji Katika Mwaka wa Fedha 2025 - 2026.
Vyeti hivyo vilikabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Dkt. Ikupa Harrison Mwasyoge wakati wa Kikao kazi cha kuweka mikakati ya kuboresha ukusanyaji wa mapato kwa Mwaka huu wa Fedha wa 2025 - 2026 , kikao hicho kilifanyika Katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri.
Katika Kikao hicho mbali na Uongozi kuwatambua wakusanyaji Bora wa mapato kwa Mwaka wa fedha uliopita, lakini pia ilifanyika tathmini mwenendo wa mapato Katika Mwaka wa fedha 2024 - 2025.
Akizungumza wakati wa Kikao hicho, Dkt. Mwasyoge aliwataka watumishi hao kukusanya mapato kwa bidii, ili kila Mmoja aweze kufikia malengo ya ukusanyaji waliyowekewa kwa Mwaka wa fedha 2025 - 2026.
Katika Mwaka wa fedha 2024 - 2025 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto ilifanikiwa kuvuka lengo kwa kukusanya zaidi ya Asilimia 100 ya mapato ambayo yalikadiriwa kwenye bajeti.
Watendaji Kata na Maafisa Ugani ambao walikabidhiwa vyeti ni kutoka Kata za Shume, Manolo, Lukozi, Lushoto, Kwai, Kilole, Ngwelo, Malindi na Magamba.
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa