- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
Kitengo cha Teknolojia ya Habari na mawasiliano (TEHAMA) ni moja wapo ya Vitengo sita na Idara kumi na mbili zinazounda Halmashauri ya Lushoto chini ya Mkurugenzi na Baraza la madiwani.Kimuundo kitengo cha TEHAMA ni Kitengo kinachojitegemea kwahiyo kitengo hiki kinaongozwa na Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA ambaye anaripoti moja kwa moja kwa Mkurugenzi Mtendaji na ndiye mshauri mkuu wa Mkurugenzi Mtendaji katika maswala yote ya TEHAMA. Kazi kubwa ya kitengo hiki nikusimamia mifumo na vifaa vyote vya TEHAMA katika Idara zote za Halmashauri. Vifaa vya TEHAMA ambavyo vinasimamiwa na kitengo cha TEHAMA ni kama ifuatavyo:- Personal computers, Computer mpakato(Laptop),printers , scanners, photocopier machine,UPS, Biometric mashine, vifaa vya network kama vile switch, router, modem, data rack,miundombinu ya mitandao ya ndani(LAN) pamoja na vifaa vya TEHAMA kitengo kinasimamia mifumo mbalimbali kama vile:- Mfumo kuandaa bajeti na kutoa taarifa (planrep), Mfumo wa ukusanyaji mapato ya serikali katika serikaliza mitaal(Local government revenue collection information system-LGRCIS).Mfumo wa kusimamia malipo na matumizi katika serikali(epicor),Mfumo wa kusimamia rasilimali watu(human capital management infoomation system-HCMIS) ,Mfumo wa kusimamia matumizi ya fedha za serilali katika vituo vya kutolea huduma kama vile hospitali,vituo vya afya ,Zahanati ,shule za msingi na sekondari (FFARS),Mfumo wa taarifa za vifaa na wanafunzi katika shule za elimu msingi na sekondari(BEMIS),Mfumo wa kutunza taarifa za wanafunzi wa shule za Msingi (PreM),Mfumo wa kutunza taarifa za wanafunzi wa shule za Sekondari (PreMS),Mfumo wa madai na madeni ya watumishi(MADENIMIS),Mfumo wa taarifa za wagonjwa,dawa na vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za afya(GoT-HoMIS) ,Mfumo wa Vibali vya Kusafiri nje ya nchi, Mfumo wa ugawaji Vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo na Mfumo selform kwa ajili ya taarifa za shule za sekondari.
MIUNDOMBINU YA TEHAMA
Miundombinu ya TEHAMA imeimarika katika ofisi zote za Halmashauri ambazo ziko katika ofisi kuu ya Halmashauri ambayo ni jengo lenye ghorofa tatu zenye watumishi zaidi ya elfu moja . Kila ofisi mifumo ya data na voice imesimikwa.Ofisi zote za wakuu wa Idara zimeunganishwa na simu za ndani(intercommunication) kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano ya ndani kwa wakuu wote wa Idara
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa