- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
HALMASHAURI ya Wilaya ya Lushoto kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam imeendesha mafunzo maalum kwa Waongoza Watalii, lengo likiwa ni kuboresha huduma za utalii na kukuza ujuzi wa mawasiliano ya kitaaluma kwa wahudumu wa sekta hiyo muhimu.
Mafunzo hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Mikutano uliopo ndani ya jengo la Kituo cha Taarifa za Utalii, Nyerere Square, Wilayani Lushoto, yakihusisha waongoza watalii kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.
Akifungua rasmi mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Dkt. Ikupa Harrison Mwasyoge, alimshukuru Mwezeshaji wa mafunzo hayo, Rachel Mwalujobo kwa kuichagua Lushoto, huku pia akiwashukuru Waongoza watalii waliokubali kushiriki mafunzo hayo.
Dkt. Mwasyoge, pia aliendelea kumshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuifungua sekta ya Utalii nchini kutokana na sera za Serikali yake ya Awamu ya Sita.
Pia, Dkt. Mwasyoge alitumia fursa hiyo kuwaasa Vijana kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani, huku akiwataka kujitokeza Kupiga Kura Oktoba 29, 2025 Katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.
Mada kuu ya mafunzo ilikuwa Ujuzi wa Mawasiliano Kitaalam ambapo washiriki walifundishwa mbinu mbalimbali za kuwasiliana kwa ufanisi, kuelewa tofauti za kitamaduni, na jinsi ya kutoa taarifa sahihi kuhusu vivutio vya utalii kwa njia ya kitaaluma na yenye mvuto.
Akizungumza Katika mafunzo hayo, Bi. Rachel Mwalujobo alisema kwamba ni muhimu kwa Waongoza watalii kuwajua wageni na tamaduni zao kwenye Mawasiliano huku akisisitiza kuwa kuwa mawasiliano bora ni msingi wa huduma zenye ubora katika sekta ya utalii.
Lushoto ni moja ya maeneo yenye vivutio vya kipekee vya utalii nchini Tanzania, vikiwemo mandhari ya kuvutia ya milima ya Usambara, maporomoko ya maji, misitu na urithi wa kiutamaduni. Kupitia uwekezaji katika mafunzo na uboreshaji wa huduma, Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto inalenga kuongeza mchango wa utalii katika uchumi wa wananchi.
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa