- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
HALMASHAURI ya Wilaya ya Lushoto, kupitia Idara ya Afya na Ustawi wa Jamii imewaaga watumishi 19 wa idara hiyo waliostaafu utumishi wa Umma kwa vipindi tofauti tofauti, Katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Ukumbi Roman Wilayani Lushoto.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Dkt. Ikupa Harrison Mwasyoge aliwashukuru watumishi hao kwa Utumishi uliotukuka huku akiwatakia kila la kheri kwenye maisha yao nje ya Utumishi wa Umma.
Dkt. Mwasyoge pia alitumia fursa hiyo kuwausia watumishi wa Umma ambao bado wako makazini kuendelea kufanya kazi kwa weledi ili na wao waweze kumaliza maisha yao ya Utumishi wa Umma salama.
Watumishi waliostaafu ni pamoja na Rose Chambo, Matulo Sembe, Mwafizei Singano, Suzana Watae, Twalibu Selenda, Eileen Magambo, Mariam Msagati, Furahini Shebila, Christina Gembe, Batuli Singano, Majibu Hassani, Joackim Shemakanka.
Wengine ni Hamis Semauya, Zakati Nguruwe, Mwanaidi Msangi, Zuwena Makamba, Biasha Kilua, Fatuma Hussein na Rukia Shekomba. Watumishi hawa wamestaafu kwa vipindi tofauti tofauti na pia walikuwa kwenye kada mbalimbali kuanzia wauguzi, madereva na walinzi.
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa