- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
IDARA YA UTUMISHI NA UTAWALA
Idara ya Utumishi na Utawala ni miongoni mwa Idara zilizomo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto iliyoanzishwa rasmi tarehe 29/06/2017 kutokana na mabadiliko yaliyofanyika katika utekelezaji na mafanikio ya awali ya matakwa ya sheria za Serikali za Mitaa ya Mwaka 1962 kifungu cha 333 iliyopitishwa na Bunge la Tanganyika. Kutokana na ukubwa wa eneo la Kiutawala, Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto iligawanywa na kupata Halmashauri mbili zinazojitegemea (Lushoto na Bumbuli) hili lilifanyika Mwaka 2012.
MAENEO YA KIUTAWALA.
Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto una Majimbo Mawili (2) ya Uchaguzi, Jimbo la UChaguzi Lushoto na Jimbo la UChaguzi Mlalo, Zipo Tarafa 5 na Kata 33, Vijiji 125, Vitongoji 948 na Mitaa ipatayo 9.
Vilevile Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto ina jumla ya Watumishi wa Umma wapatao 3412 ambao wote hawa wapo kwenye Idara zilizopo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Idara nyingine ni kama vile Afya, Elimu (Msingi na Sekondari)Kilimo, Ushirika na Umwagiliaji, Mifugo na Uvuvi, Ujenzi, Ardhi Maliasili na Misitu, Maendeleo ya Jamii, Fedha na Mipango na Uchumi. Pia vipo vitengo kama vile Sheria, Mazingira, Utawala Bora, TEHAMA, Biashara na Mapato, pamoja na Nyuki.
Idara hizi zote hufanya kazi na kuwajibika moja kwa moja kiutumishi kupitia Idara ya Utumishi na Utawala.
MALENGO YA IDARA.
MAJUKUMU YA IDARA.
MAMBO MENGINE MUHIMU YANAYOFANYIKA.
Idara ya Utumishi na Utawala ya Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto hutekeleza majukumu yake kwa kufuata na kuzingatia kanuni na misingi ifuatayo
MAFANIKIO YA IDARA:
Kuondoa tatizo la watumishi kutolipwa Mishahara yao kutokana na kuwepo kwa mfumo wa kuwaingiza kwenye Pay roll na kuwafuta ndani ya mfumo wa Pay roll watumishi wanaostaafu kufariki na kuhama.
CHANGAMOTO ZILIZOPO.
Matatizo katika mfumo punde panapotokea kukatika kwa Umeme na Mtandao unapokuwa chini.
DIRA YA HALMASHAURI:-
Kuwa na jamii yenye uwezo wa kufikia huduma bora na endelevu za Kijamii na kiuchumi ili kuwa na maisha bora kwa kila mtu ifikapo Mwaka 2025
DHAMIRA YA HALMASHAURI :
Kutoa huduma bora za kijamii na kiuhcumi kwa kutumia rasilimali zilizopo kupitia Utawala Bora.
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa