- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
Historia ya uwanzishwaji wa wilaya ya Lushoto sambamba na Halmashauri ya Lushoto
Kuthubutu katika kujiletea maendeleo kulianza mara baada ya kuvunjwa kwa eneo la kiutawala lilloachwa na wakoloni kabla ya uhuru ambalo lilijulikana kama " province",eneo hili lilijumuisha wilaya ya Korogwe,Handeni,Kilindi , Same,na Mwanga.Mabadiliko hayo yalifanyikaikiwa ni hatua muhimu ya Utekelezaji wa mafaniko ya awali kabisa ya matakwa ya sheria za serikali za mitaa ya mwaka 1962 kifungu cha 333 iliyopitishwa na Bunge la Tanganyika wakati huo.Mabadiliko hayo yalizaa wilaya mpya ya Lushoto ilikwenda sambamba na uanzishwaji wa Halmashuri ya Lushoto rasmi tarehe 29 Juni 1962 kabla haijagawanyika tena na kuzaa Halmashauri mbili Lushoto na Bumbuli Mwaka 2013.
Eneo la Utawala
Halmashauri ya Lushoto ipo kaskazini mwa Mkoa wa Tanga kati ya Latitude 4 25'-4 55' kusini mwa Ikweta na Longitude 30 10'-38 35' Mashariki mwa Longitudo kuu.Kijiografia wilaya Wilaya imepakana na nchi ya Kenya kwa upande wa kaskazini Mashariki,Wilaya ya Same (Mkoa wa Kilimanjaro Kwa upande wa kaskazini Magharibi,Wilaya ya Korogwe kwa upande wa kusini ,Halmashauri ya Bumbuli upande wa kusini Mashariki ,Kwa upande wa Mashariki ya mbali imepakana na Muheza na Mkinga
Halmashauri ya Lushoto inaeneo la ukubwa wa kilometre za mraba 2,300 km2 ( Hekta 227,371.43) sawa na asilimia 8.41 ya eneo lote la mkoa wa Tanga
Utawala
Halmashauru ina Tarafa 5 Kata 33 vijii 134 pamoja na Vitongoji 948. Makao makuu ya Halmashuri ya Lushoto yako Mjini Lushoto. Halmashauri imegawanyika katika majmbo mawili ya Uchaguzi Lushoto na Mlalo.
Dira
Nikuwa na Jamii yenye uwezo wa kufikia huduma endelevu za jamii na kiuchumi
Dhima
Kutoa huduma bora za kijamii na kiuchumi kwa kutumia rasilimali zilizopo kupitia Utawala bora
IDADI NA MTAWANYIKO WA WATU KATIKA MAENEO MBALI MBALI YA HALMASHAURI YA LUSHOTO
Demografia ya Halmashauri ya Lushoto ilikuwa ikiongezeka kwa ukubwa tangu 2012 kutoka 332,436 mpaka 350,958 mwaka 2022, Katika sensa ya 2012 Halmashauri ilikuwa ina idadi ya watu 332,436(153,844 wakiwa wanaume) na (178,589 wakiwa wanawake) katika sensa ya mwaka 2022 Halmashauri ya Lushoto ina idadi ya watu 350,958 (160,815 wakiwa wanaume na 190,143 wakiwa wanawake).
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa