- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Lushoto anapenda kuwatangazia wananchi na wakazi wa Halmashauri ya Lushoto kwamba mwenge wa Uhuru utafanya mbio zake ndani ya Halmashauri ya Lushoto tarehe 03.10.2018 , Mwenge wa Uhuru utapokelewa mkomazi na kukimbizwa kupitia kata za Mnazi, Lunguza ,Mg'aro, Kwemshasha Mlalo Mwangoi, Malindi magamba hatimaye Lushoto.
Mwenge wa uhuru pia utapitia miradi minne kama vile Kiwanda cha kuchakata zao la mkonge, Maabara ya Kemia shule ya sekondari ya kwemaramba,Ujenzi wa upanuzi wa miundombinu wa kituo cha Afya cha Kangagai na Mradi wa utunzaji wa mazingira wa '' Friend of Usambara'' na jioni ya tarehe 3.10.2018 kwenye mkesha wa mwenge wa uhuru katika uwanja wa sabasaba mjini Lushoto wananchi wote mnakaribishwa.
Pia mwenge utakuja na kauli mbiu isemayo " ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA WEKEZA SASA KWA MAENDELEO YA TAIFA LAKO"
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa