- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
UTARATIBU WA KUPATA LESENI ZA BIASHARA
Wizara ya viwanda na biashara ambayo inasimamia moja kwa moja shughuli za viwanda na biashara hapa nchini imetoa maelekezo ya kufuata katika zoezi lakutoa leseni kwa wafanya biashara chini ya sheria ya leseni za biashara namba 25 ya mwaka 1972 na marekebisho yake. Ufuatao ni utaratibu wa kufuata katiak utoaji wa Leseni za Biashara zilizopo kwenye kundi B kama zinavyosimamiwa na mamlaka za serikali za mitaa ;
Mfanyabiashara anatakiwa kuwa na taarifa za kuonyesha analipa mapato(Tax clearance) kutoka Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA).
Kuwa na uthibitisho wa kibali kutoka mamlaka Husika kwa mfano; Biashara ya Hotel,migahawa,butcher kutoka kwa Bwana Afya, Biashara ya mziki (Disco) kutoka BASATA, Duka la madawa kibali toka TFDA n.k
Kulipa Ada ya Lesseni kulingana na aina ya Biashara.
Baada ya kukamilisha taratibu zote Mteja/Mfanyabiashara atapatiwa Lesseni ya Biashara ndani ya masaa 24.
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa