- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
MKUU wa Wilaya ya Lushoto, Mhe. Kalisti Lazaro amekagua zoezi la uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza siku ya kufungua shule Januari 8, 2024 ili kuona mwitikio wa wazazi na walezi kwenye kuripotisha watoto shuleni, huku pia akitaka kujua changamoto zilizopo katika kufanikisha zoezi hilo.
Akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mhe. Lazaro alipata wasaa wa kuzungumza na wazazi na walezi waliojitokeza katika shule ya msingi Mbula B na shule ya Sekondari ya Shambalai, ambapo aliwaeleza kwamba elimu ni bure katika shule zote za serikali hivyo wasisite kuwaripotisha shule watoto waliotimiza umri wa kuanza shule.
"Serikali ya Mama Samia (Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan) imeshatimiza wajibu wake, kwa kuandaa miundombinu yote iliyohitajika kupokea watoto wa darasa la awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza wiliayani Lushoto, hakuna mwanafunzi hata mmoja atakayekosa darasa wala dawati, kazi iliyobaki ni wazazi kupeleka watoto shule." Alisema Mhe. Lazaro.
Mhe. Lazaro aliendelea kusisitiza kwamba hakuna masharti au kikwazo chochote kwa mtoto kutokwenda shule, huku akiwataka wazazi kumfikishia taarifa iwapo watakutana na kikwazo chochote kutoka kwa mwalimu pindi wakienda kuandikisha watoto, kwa sababu gharama zote za Elimu tayari Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshalipia
Katika hatua nyingine, Mhe. Lazaro amesema hatasita kuwachukulia hatua kali za kisheria wazazi ambao watashindwa kwende kuwaandikisha shule watoto waliofaulu kuendelea na masomo ya sekondari, ambapo aliweka wazi kuwa ofisi yake inajua walipo wanafunzi wote ambao wamefaulu kuendelea na kidato cha kwanza.
"Serikali inafahamu ni wapi walipo watoto wote waliofaulu kuendelea na kidato cha kwanza, hivyo mzazi usipomleta mwanao shule, tutatumia taarifa zilizopo katika shule ya msingi aliyosoma mtoto wake, na tutakusaka popote ulipo na safari hii tutakiwakamata tutawapanisha mahakamani." alisema Mhe. Lazaro.
Akiwa Shule ya Msingi Mbula B, Mhe. Lazaro, alipewa taarifa kwamba shule hiyo imevuka lengo la uandikishaji kwenye darasa la awali na darasa la kwanza, ambapo katika darasa la awali walikuwa lengo la kuandikisha wanafunzi 120, lakini katika siku ya kwanza tu walikuwa wameandikisha wanafunzi 147.
Wakati kwa darasa la kwanza walikuwa na lengo la kuandikisha wanafunzi 70, lakini katika siku ya kwanza tu ya uandikishaji tayari walikuwa wameshaandikisha wanafunzi 84, huku wengine wengi wakiwa wameletwa na wazazi wao kwa ajili ya kukamilisha zoezi la uandikishaji.
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa