- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
MKUU wa Wilaya ya Lushoto, Mhe. Kalisti Lazaro amewataka wananchi wanaoishi kwenye mazingira hatarishi kuhama katika maeno haya ili kujiepusha na maafa hasa katika kipindi hiki ambacho mvua nyingi zimeendelea kunyesha katika Wilaya hiyo na nchi nzima kwa ujumla.
Ameyasema hayo akiwa wakati alipotembelea Kata ya Lunguza na Mbaramo akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ili kuona uharibifu uliojitokeza katika maeneo hayo kufuatia mvua nyingi zilizonyesha kwa siku tatu mfululizo kuanzia tarehe 7/1/2024 hadi tarehe 9/1/2024 na kusababisha uharibifu wa mali na vifo vya watoto wawili wa familia moja.
Akizungumza baada ya kufika eneo la tukio Mhe. Lazaro alisema kwamba tayari serilikali kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa ilishasema kwamba mwaka huu tutarajie mvua za El Nino, hivyo ni wajibu wa wananchi kuhama kutoka kwenye maeneo hatarishi ili kujiepusha na maafa yanayoweza kujitokeza.
Mhe. Lazaro aliendelea kuwasisitiza wananchi kuwa makini na maji yanayotembea huku akiwataka wazazi kuwasindikiza watoto shule ili kuwalinda na hatari wanayoweza kukutana nayo wakiwa njiani hasa katika kipindi hiki ambacho barabara nyingi zimejaa maji yanayotembea.
Katika hatua nyingine; Mhe, Lazaro alitoa pole kwa Wananchi wa Kijiji cha Wangwi, Kata ya Mbaramo kufuatia vifo vya watoto wawili wa familia ya Ndg. Tulo Emanuel Shemndolwa ambavyo vilitokea Usiku wa kuamkia tarehe 10/1/2024, baada ya kuangikiwa na ukuta wa nyumba wakiwa nyumbani wamelala.
Mhe. Lazaro alisema hadi sasa Lushoto hakuna kesi ya mafuriko makubwa na badala yake nyumba nyingi zilizoanguka kwenye Kata ya Lunguza na Mbaramo zinatokana na kujengwa chini ya kiwango, hivyo kushindwa kuhimili maji kutokana na mvua kubwa ambazo zinaendelea kunyesha kwenye maeneo hayo.
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa