- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
Kata mbili, ambazo ni Kata ya Mlola na Kata ya Makanya zilizopo katika wilaya ya Lushoto. Tarehe 06/10/2021 zimepata ugeni wa viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Lushoto na pia ugeni Kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto. Ikiwa ni ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo na kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa wilaya ya lushoto inayofanywa na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Mh Karist Lazaro.
Ziara iyo ilianzia Kata ya Mlola katika Kijiji cha Ungo ambapo kulikua na Mradi wa Maendeleo wa jengo moja ambalo lina madarasa mawili ya kusomea wananafunzi.
Ziara ikaendelea mpaka kwenye Kijiji cha Mazashai kwenye Shule ya Msingi Mgambo ambayo ni Shule Shikizi Kutoka Kwenye Shule Mama, Shule ya Msingi Mazashai. Katika shule hiyo ya Mgambo, Mh. Karist Lazaro alikagua Majengo Mawili kila moja likiwa na Vyumba viwili vya Madarasa. Shule iyo Shikizi imeanzishwa kwa Lengo la Kuondoa Kero kwa Wanafunzi ambao walikua wanalazimika kutembea umbali mrefu mpaka kwenda kufika shule ya Msingi Mazashai. Mh. Karist Lazaro aliwapa nafasi wananchi wa Kijiji icho kusema kero zao, wanakijij ao walikua na Ombi la Kuongezewa Walimu katika Shule hiyo ambayo ina idadi ndogo ya walimu.
Kijiji cha Lwandai, Mh Karist Lazaro alikagua Miradi Miwili kwenye shule ya Sekondari Mlongwema na Ujenzi wa Chuo cha Veta.
katika Shule ya Sekondari Mlongwema, Mradi uliokaguliwa ni Maabara ya Sayansi. Na pia Kwenye Chuo cha Veta alikagua Majengo yote ya chuo icho ambayo Bado ujenzi unaendelea.
Zahanati ya Kijiji cha Mdando, Mh Karist Lazaro aliendelea na Ziara mpaka kwenye kijiji cha Mdando ambapo alikagua jengo la Zahanati ya Kijiji icho cha Mdando ambalo limejengwa kwa Nguvu za Wananchi wa kijiji icho cha Mdando.
Kijiji cha Bwaya. katika kijiji cha Bwaya, katika Shule ya Msingi Bosha. Ambapo alikagua Jengo moja lenye Madarasa Mawili ya kusomea wanafunzi.
Mwisho wa ziara ulikua ni Katika Kata ya Makanya, katika kata iyo, Mh Karist Lazaro alitembea Maeneo Mbalimbali na alitoa usuruhishi katika kero mbalimbali za Wananchi wa Kata iyo ya Makanya na baadae aliweka Mkutano wa Azara Kwenye uwanja wa Ofisi za Chama cha Mapinduzi(CCM) Kweurasi, ili kuongea na wananchi na Kusikiliza na Kutatua Kero mbalimbali za Wananchi. Katika mkutano uo wananchi walitoa kero zao na kuuliza Maswali mbalimbali ambayo yalijibiwa na Wataalam, Wakuu wa Idara Mbalimbali na Wakuu wa Taasisi mbalimbali
Katika ziara iyo Mkuu wa wilaya ya lushoto, Mh. Karist Lazaro aliongozana na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Lushoto, Mbunge wa jimbo la Lushoto, Mh. Shaban Shekilindi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Lushoto, Mh. Methew Mbaruku, Diwani wa Kata ya Mlola, Mh. Ramadhan Mkamba na Diwani wa kata ya Makanya, Mh. Zanieri Kipingu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Bi. Ikupa Harrison Mwasyoge, Wakuu wa Idara mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto na Wakuu wa Idara wa Taasisi Mbalimbali.
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa