- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Lushoto Mh.Methew Mbaruku awaongoza madiwani wote wa Halmashauri kwenye kikao cha baraza kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri tarehe 29/4/2021. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mh .January Lugangika ,mwakilishi kutoka ofisi ya RAS Tanga, wakuu wa Idara wakiongoza na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Bi.Ikupa Harrison Mwasyoge,Ma maneja kutoka taasisi mbalimbali za serikali kama vile Tanesco, Luwasa , Mahakama , wawakilishi wa vyama vya siasa pamoja na baadhi ya wananchi wa wilaya ya Lushoto.
Katika Kikao hicho Mkuu wa wilaya ya Lushoto aliiitolea ufafanuzi wa salamu maaalum ya Jamhuri ya Muungano ya kazi iendelee katika kusimamia uchumi wa kati tulioupata hivi karibuni,mipango yote maendeleo na miradi ya kimkakati iweze kukamilika kwa wakati,kutekeleza ilani ya chama tawala na ulinzi na usalama. na kufanyakazi kwa bidii na uaminifu. Pia katika kikao hicho aliwasihi madiwani kuhakikisha mikutano yote ya kisheria katika ngazi ya kata na kijii inafanyika kalingana na ratiba zao na wanahudhuria mikutano hiyo ili kuitolea ufafanuzi baadhi ya hoja.Mkuu wa wilaya pia aliwasihi madiwani wanasimamia kilimo katika kata zao,wanatatua migogoro ya wafugaji na wakulima,
Katika elimu Mkuu wa wilaya alisisitiza umuhimu wa chakula cha mchana mashuleni hasa hasa shule za msingi na kuwasihi waheshimiwa madiwani kuwahimiza wazazi kuchangia gharam za chakula kwa watoto wao.Katika kipindi hiki cha baridi wanafunzi washonewe nguo za kuzuia baridi kama vile suruali na ijabu kwa wanafunzi wa kike na niwajibu wa wazazi kuhakikisha wanagharamia .Kuhusu miundombinu na vyanzo vya maji vilivyo katika kata zao mkuu wa wilaya ya Lushoto aliwasihi waheshimiwa madiwani wanawaelekeza wananchi umuhimu wa kutunza miundombinu kwani serikali inatumia fedha nyingi kuijenga.
Kuhusu vyombo vya habari mweshimiwa mkuu wa wilaya aliwashukuru kwa kazi nzuri wanayo ifanya na waendelee kutanga mambo yote mazuri yanayofanywa na Halmashauri.Baada ya salamu za Mkuu wa wilaya taarifa mbalimbali za utekelezaji shughuli za maendeleo katika robo ya tatu ziliwasilishwa na wenyeviti wa kamati mbalimbali za Halmashauri zikiwemo
Kamati ya kudhibiti na kupambana na Ukimwi
Kamati ya Elimu Afya na Maji
Kamati ya fedha Uongozi na Mipango
Kamati ya maadili ya wah. Madiwani
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa