- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
Mweshimiwa Mkuu wa mkoa wa Tanga ndugu Martine Shigela aongoza kikao cha baraza maalum la Halmashauri ya wilaya ya Lushoto kwa ajili ya kupitia hoja za mkaguzi na mdhibiti wa Hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19. Wakati anahutubia kikao hicho aliwapongeza madiwani kwa kuisimamia vizuri Halmashauri na kuiwezesha Halmashauri kupata hati safi mfululizo na kumpogeza mwenyekiti wa Halmashuri kwa kuendesha vikao na kuwaongaza wah.madiwani kidemokrasia pia aliwakumbusha kujiepusha na migogoro ambayo inarudisha maendeleo ya Halmashauri nyuma .Pamoja na kuwapongeza pia aliwaomba kuendelea kuisimamia Halmashauri ili iongeze juhudi za kukusanya mapato kwa kuwa Halmashauri bado iko nyuma kiasilimia kulingana na malengo iliyojiwekea.Pia alitumia fursa hiyo kutoa maagizo kwa mkuu wa wilaya na Mkurugenzi kuhakikisha fedha zote zilizokusanywa na mawakala au watumishi ambazo hazijiwekwa banki kuhakikisha zinaweka banki kabla ya mwaka wa fedha kuisha. Kwa taarifa aliyokuwa nayo ilikuwa ilikuwa inaonyesha Halmashauri ya Lushoto ina kiasi cha sh .milion tatu za kitanzani (3,000,000) ambazo hazija pelekwa benki kiasi ambacho kinaonekana kuwa kidogo ukilinganishwa na Halmashauri nyingine na kuipongeza Halmashauri kwa hilo.
Mweshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga alitoa maelekezo mbalimbali kwa Halmashauri kuhakikisha madeni yao yote yanalipwa kabla ya kipindi chao cha uongozi kufikia tamati au mwisho ili wakistaafu waone fahari kuitumikia Halmashauri na kuhakisha mikopo ambayo wameingia kwa udhamini wa Halmashauri inalipwa ili watakapokuwa wamestaafu wasifatwefatwe na maafisa wa banki kudai marejesho ya mikopo yao waliochukuwa wakati wanaitumikia Halmashauri.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga alitoa maelekezo kwa Halmashuri kuhakikisha zile asilimia kumi ya mikopo ya wanawake na vijana inapelekwa kwa walengwa kulingana na miongozo iliyopo pia kuhakikisha marejesho ya mikopo hiyo inafatiliwa na inarejeshwa kwa wakati na kuisifia Halmshauri kuonyesha jitihada za kutoa mikopo hiyo na kuhimiza juhudi hizo ziongezeke nakuifatilia mikopo hiyo na kuhakikisha inarejesha kwa wakati ili iweze kusaidia watu wengine.
Pia mkuu wa mkoa alitolea ufafanuzi mzuri wa mchakato mzima wa uuzaji wa shamba la mnazi baada ya mchakatoa huo kunugunikiwa na baadhi ya wanasiasa ikiwemo madiwani pia kujitokeza kwenye hoja za CAG. Mkuu huyo wa mkoa wakati anatoa ufafanuzi alibainisha kuwepo kwa upungufu(vacuum) wa kutotoa taarifa sahihi kwa wahusika hali iliyopelekea watu kutengeneza taarifa zao zisizo sahihi na kupelekea minogono isiyokuwa na tija katika Halmashauri na kupelekea baadhi ya watumishi kufukuzwa kazi na baada ya ufanuzi huo wajumbe walionyesha kulidhika na maelezo ya Mh.Mkuu wa Mkoa na kuelekeza mchakato mzima ukamilike ikiwa ni pamoja na kupima hilo shamba ili serikali iweze kupata mapato yake pia na kuuza viwanja na Halmashauri iweze kuongeza mapato
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa