- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
Mkuu wa wilaya ya Lushoto Mh. Januari Lugangika ametoa onyo kali kwa makandarasi wote wanaofanya kazi katika wilaya ya lushoto katika kutekeleza mirandi mbalimbali ya maendeleo alipokutana nao kwenye kikao cha pamoja na wajumbe wa bodi za zabuni ili kuhakikisha miradi hiyo ikamilike kwa wakati na ubora unaotakiwa.
Katika kikao hicho alikemea vikali suala la rushwa kati ya wakandarasi na bodi zinazotoa zabuni za ujenzi, kwani kumekuwa na kulegalega kwa kazi kutokana na kupewa kazi kwa maakandarasi wasio na sifa na kutokuwa na vitendea kazi vya kutosha hali hali inayosababisha kuchelesha kazi au kushindwa kumalizika kwa wakati.
Ili kukabiliana na hali hiyo Mkuu wa wilaya hata sita kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayejihusisha na vitendo hivyo ikiwa ni pamoja na kumkamata na kumweka ndani pia na kumfutia leseni yake.Wakati huo Mh. Mkuu wa wilaya alitembelea hospitali ya Walaya ya Lushoto ili kujionea mwenyewe eneo lililotengwa kama karantini ya wagonjwa wa corona.Akitoa taarifa ya maadalizi ya kukabiliana na ugonjwa wa corona Kaimu mganga Mkuu Bi Agnes Kwagilwa alisema madaktari wamejipanga na timu nzima imekamilika na huduma zitakuwa masaa 24.
Wakati huo Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Lushoto ndg Ikupa Harrison Mwasyoge akimwakilisha Mkuu wa wilaya ya Lushoto amakabidhi vifaa vilivyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Kwa waathirika wa mafuriko mwishoni mwa mwaka 2019 katika tarafa ya Mlalo wilayani Lushoto, Vifaa hivyo ni kama ifuatavyo mchele kilo 100, Maharage kilo 40 ,Mafuta ya kupikia lita 100 , magodoro 61 pamoja na shuka 41
Pia alitoa angalizo kwa wananchi wanaoishi mabondeni kuhama mara moja ili kuepukana na majanga yanaweza kujitokeza kutoka na mvua nyingi zinazotarajiwa kunyesha mwanzoni mwa mwezi April 2020.Pamoja na hayo alisisitiza kilimo cha matuta/makinga maji ili kuzuia maporomoko ya maji toka milimani.
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa