- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
Halmashauri ya wilaya ya Lushoto imefanya maadhimisho ya siku ya wanawake katika kata ya Mbwei kijiji cha mbwei kwa lengo la kuchochea maendeleo katika kata ya mbwei kupitia kauli mbiu yenye ujumbe wa mwaka 2020, "KIZAZI CHA USAWA KWA MAEDELEO YA SASA NA BAADAYE." Maadhimisho haya yanatoa fursa za kuonyesha mafanikio na changamoto zinazowakabili wanawake na jinsi ya kuzitatua kwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo.Ili kutimiza hazima hiyo Halmashauri imefanikiwa kutoa mikopo kwa vikundi 81 vya wanawake tangu mwaka 1996 -2020 . Kutokana na mikopo hiyo familia za wanawake hao zimeweza kusomesha watoto wao ,kujenga nyumba bora na kuongeza kipata.Baadhi ya vikundi vilivyo nufaika na makopo viliweza kuleta bidhaa zao na mifungo na kuviuza wakati wa kilele cha sherehe ya siku ya wanawake ambapo mgeni rasmi alipata fursa ya kupitia kila kikundi na kupata maelezo ya jinsi kila kikundi kinavyo endesha biashara zake hususani utunzaji mzuri wa fedha zinazopatika ili kuzifanya biashara hizo ziwe endelevu.
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa