- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
Mkandarasi wa Kampuni ya BULLEM INVESTIMENT LTD akabidhi jengo la soko la mbogamboga la mnadani lililoko kata ya malindi wilayani Lushoto lenye thamani ya sh.1,045,500,861,Mradi wa ujenzi wa Jengo la soko mnadani ulianza kutekelezwa mnamo mwaka 2011 kwa rusuku ya maendeleo inayotolewa na serikali kuu(CDG) na mapato ya Halmashauri ukiwa ni mradi wa kata ya malindi.
Soko hili baada ya kukamilika litakuwa na matumizi mbalimbali kama ifuatavyo:
SEHEMU YA CHINI YA JENGO(GROUND FLOOR)
Sehemu hii inavizimba au meza thelathini (30) ambavywo vitatumiwa na wafanyabiashara wa rejareja ambao watauza mazao ya mbogamboga, na itakuwa na Ofisi za soko na upande wa nyuma wa sehemu hii una ghala lenye uwezo wa kuhifadhi tani 100 kwa wakati mmoja,
SEHEMU YA GOROFA YA KWANZA (FIRST FLOOR)
Sehemu hii inavyumba vya baridi (Cold room) kwa ajili ya kuifadhi mazao ya mbogamboga kabla ya kupelekwa kwenye masoko au kuhifadhi mbogamboga wakati wa msimu ambapo mboga hizo zinakuwa nyingi na kukosa soko na mkulima kupata hasara kama ataziuza kwa kipindi hicho kwa kuogopa kaharibika badala yake itazihifadhi kwenye vyumba hivywo vya baridi (cold room) mpaka hapo bei itakapokuwa nzuri sokoni na mkulima akauza kwa faida. vyumba hivywo viko viwili na kila kimoja kina uwezo wa kuhifadhi kreti 130 za mazao kwa wakati mmoja .Pia sehemu hii ina meza sita za kuchambua mazao kabla ya kuifadhiwa kwenye vyumba vya baradi(cold room).
SEHEMU YA GOROFA YA PILI (SECOND FLOOR)
Sehemu hii imejengwa kwa matumizi mbalimbali kutegemeana na hitaji la wakati husika mfano linaweza kutumika kama ukumbi wa mikutano au sherehe au linaweka vibanda vya biashara na pia sehemu hii ina eneo la Mgahawa na maliwato na sehemu ya wazi kwa ajili ya kupumzikia
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa