- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
Mbio za mwenge wa uhuru zimehitimishwa katika Halmashauri ya lushoto, Mwenge huo ulianza kukimbizwa katika Halmashauri ya Lushoto ukitokea Halmashauri ya Bumbuli kuanzia tarehe 14/6/2023 mpaka tarehe 15/6/2023 baada ya kuukabidhi katika Halmashauri ya Korogwe saa tatu kamili. Mwenge huo ukiwa katika Halmashuri ya Lushoto umekimbizwa takrabani KM 173 na umetembelea,kuwekea na kufungua jumla ya miradi nane, kati ya hiyo miradi mitatu ilifunguliwa ,mitatu mengine iliwekewa jiwe la msingi na miwili kutembelewa.
Pamoja na kutembelea kukagua, kuwekekea jiwe la msingi na kufungua miradi yenye thamani ya zaidi ya bilioni moja kiongozi wa mwenge wa uhuru kitaifa ndugu Abdalla Shaib Kaim alifafanua vizuri kauli mbio ya mwenge wa Uhuru 2023 kwa wananchi wa Halmashauri ya lushoto ambayo ilikuwa inasema mabadiliko ya tabia nchi ,Hifadhi ya mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji"Tunza mazingira ,okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai kwa uchumi wa taifa "
Pia mwenge huo umepitia katika tarafa mbili kata nane na vijiji ishirini na tatu na miradi mikubwa iliyofunguliwa na kuweke jiwe la msing ni pamoja mradi mkubwa maji irente yoghoi ngulwi bombo, zahanati,choo cha kisasa cha shule ya msing Lushoto , kituo cha mafuta cha parengo ,na daraja la mlesa katika Halmashauri ya Lushoto
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa