- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Lushoto Mh.Lucas Shemdolwa aongoza kikao maalum cha kupitia na kujadili hoja za mkaguzi na mdhibiti wa Hesabu za Serikali(CAG) pamoja na maagizo ya LAAC kabla ya hoja hizo kupelekwa kwenye kamati maalum ya bunge anayoshughulika hesabu za serikali za mitaa (LAAC). Katika kikao hicho jumla ya hoja thelathini na sita(36) ziwasilisha pamoja na maagizo ishirini na sita (26) ya LAAC yaliyotolewa na wakati wa kujadili taarifa ya mdhibiti na mkuguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) kwa mwaka 2014/15.Katika kikao hicho wah. Madiwani walipitia hoja moja baada ya nyingine na kupitia majibu ya manejimenti kisha maoni ya kamati ya ukaguzi na kamati ya fedha kisha kutoa maoni yao kama baraza la madiwani . Hoja ambazo zilionekana zinahitaji ufafanuzi zaidi kikao hicho kiliagiza ziletwe kwenye kikao cha kamati ya fedha na mipango ili ziweze kujadiliwa kwa muda mrefu zaidi na kupatiwa ufafanuzi zaidi.Pia katika kikao hicho kirihudhuriwa na katibu tawala wa mkoa wa Tanga ambaye alitumia muda huo kujitambulisha kwa waheshimiwa madiwani kwakuwa hicho kilikuwa kikao chake cha kwanza kukihudhuria katika Halmashauri ya Lushoto tangu ateuliwe na Mh. Rais wa Jamhuri wa Tanzania kushika widhifa huo katika Mkoa wa Tanga.Ras aliwapongeza sana wabunge wote kwa michango yao mahili iliyoonyesha madiwani kuifahamu vizuri Halmashauri yao kwa kuisimamia vizuri na kuweza kujenga jengo zuri sana kwa ajili ya watumishi wote wa Halmashauri walioko makao makuu ya Halmashauri.
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa