- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Lushoto Mh. Methew Mbaruku aongoza kikao cha baraza la madiwani cha robo ya pili katika ukumbi wa Halmashuri ya Lushoto tarehe 25/2/2023.Kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali wakiongozwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, kwa upande wa chama tawala kiliwakilishwa na mwenyekiti wa chama wa wilaya na katibu wake ,Mkurugenzi wa Halmashauri ,wataalamu mbalimbali kutoka ofisi ya Mkurugenzi wakiongozwa na wakuu wa Idara na vitengo,Maneja wa maji wa wilaya na taasisi mbalimbali zilizoko katika wilaya, viongozi wa vyama vya siasa, Pia kikao hicho kilihudhuriwa na Mbunge wa Mlalo Mheshimiwa Rashid Shangazi.
Katika kikao hicho wajumbe walisoma na kudhibitisha muhtasari wa kikao cha robo ya kwanza ya baraza kilichofanyika tarehe 29/11/2022 ,wajumbe waliupitia na kurekebisha makosa ya kimantiki kisha kuupitisha kuwa kumbukumbu ya kudumu ya Halmashauri.
Katika kikao hicho wenyeviti wa kamati za kudumu za Halmashauri waliwasilisha mihtasari ya taarifa za kamati za kudumu za Halmashauri kwa kipindi cha robo ya pili Oct -Desemba 2022/23 kama ifuatavyo-
Mwenyekiti wa kamati ya kudhibiti na kupambana na ukimwi aliwasilisha taarifa ya kamati hiyo ikiwa na agenda tatu ambazo zilikuwa ni nikupitia utekeleza wa yatokanayo ya robo ya kwanza, utekelezaji wa shughuli za idara kwa kipindi cha robo ya pili, taarifa ya mapambono ya ukimwi toka kwa wadau kama vile LEVO,IJA,WMAC -MWANGOI, WMAC MLALO na mengineyo ikiwa ni kamati kutembelea mashule ya msingi na sekondari kukagua utoaji wa elimu ya VVU na UKIMWI
Mwenyikiti wa kamati ya elimu afya na maji naye aliwasilisha taarifa yake ikiwa na agenda mbalimbali zilizojadiliwa katika kamati yao ikiwa ni kusoma na kudhibitisha muhtasari wa kikao cha robo ya kwanza,utekelezaji wa yatokanayo na kikao cha robo ya kwanza ikiwemo kikao hicho kupata taarifa ya maboma ya zahanati ambazo zimeombewa fedha kwenye bajeti ya 2022/23 ambayo taarifa yake ilitolewa kikaoni zahanati hizo zikiwa zahanati za kwekifyinyu (msale), chumbageni , kishangazi ,kifulio na Mziragembei, agenda nyingine ilikuwa ni kujadili shughuli za utekelezaji za Idara za elimu msingi na sekondari, afya. Kazi kubwa zilizofanyika katika elimu msingi ni kusimamia ufanyikaji wa mitahani ya mihula na necta, kushiriki michezo kukagua madarasa ya UVICO. Kwa upande wa sekondari kufatilia miradi ya maendeleo ya shule za sekondari ufatiliaji wa mitihani ya upimaji ya mihula na kidato cha nne,kwa upande wa afya baadhi ya shughuli zilizofanyika ni kutoa huduma kwa familia malezi , makuzi na maendeleo ya watoto na mashauri ya ndoa.
Mwenyekiti wa kamati ya uchumi ujenzi na mazingira aliwasilisha taarifa yake kwa kipindi cha robo ya pili ikiwa na ageda mbalimbali ikiwemo kupita utekelezaji wa yatokanayo kwa kikao kilichofanyika 20/09/2022,utekelezaji wa shughuli za Idara kwa robo ya pili ambapo idara za kiliomo umwagiliaji na ushirika,maendeleo ya mifungo na uvuvi, maendeleo ya jammii jinsia watoto na wazee,usafi na mazingira,ardhi,biashara na ujenzi , maliasili na hifadhi ya mazingira na kitego cha TASAF ziliwasilisha taarifa zake za utekelezaji.
Mwenyekiti wa kamati ya fedha uongozi na mipango ambaye ni mwenyekiti wa Halmashauri aliwasilisha taarifa yake kwa kupitia makamu wake ikiwa na agenda mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa yatokanayo wa kikao cha tarehe 09/11/2022 likiwemo swala la shule zilizopelekewa sh 23,000,000/= kwa ajili ya vyoo ziweze kujulikana , utekezaji wake ulikuwa kama ifuatavyo , shule zilizopelekewa fedha hizo ni Kongei matundu matano , mshizii matundu manne, mtii matundu manne na kivingo matundu manne.
Kamati ilipokea taarifa ya mapato na matumizi kwa mwaka fedha 2022/2023 na Halmashauri ikiwa inakisia kukusanya jumla ya sh.Tsh. 46,446 ,085,826.00 kutoka vyanzo mbalimbali za mapato ikijumuisha bakaa Tsh,268,437,957.98 kutoka mwaka wa fedha 2021/2022 inafanya bajeti ya mapato yote kwa mwaka kufikia jumla ya sh.46,714,523,783.98.
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa