- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
KAMATI za Kudumu za Madiwani za Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto (Lushoto DC), Jumamosi, tarehe 18/11/2023 ziliwasilisha taarifa za Kamati hizo na kupitishwa wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani la Robo ya Kwanza la Mwaka wa Fedha 2023/2024 uliofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri.
Taarifa zilizowasilishwa kwa ajili ya kupitishwa ni za Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango, Kamati ya Kudhibiti na Kupambana na UKIMWI, Kamati ya Elimu, Afya na Maji, Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira pamoja na Kamati ya Maadili ya Waheshimiwa Madiwani.
Akiwasilisha Taarifa ya Kamati Fedha, Uongozi wa Mipango Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri; Diwani wa Kata ya Mbaramo, Mhe. Hatibu Ulanga, alisema kwamba katika Robo ya Kwanza (Julai - Septemba), Kamati ilifanya vikao vinne vya kawaida ambapo katika vikao hivyo vikao vitatu vimethibitishwa na kimoja hakijathibitishwa.
kwa mujibu wa taarifa ya Kamati hiyo, Katika kipindi cha Julai 2022 – Juni 2023, Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto ilikusanya jumla ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 46.57 kutoka katika vyanzo mbalimbali,sawa na asilimia 99.71 ya mapato ya makisio ya bajeti, ambapo Mapato ya ndani yalikuwa ni shilingi bilioni 2.37, ruzuku ya matumizi ya kawaida shilingi bilioni 1.49, mishahara shilingi bilioni 31.7 na miradi ya maendeleo shilingi bilioni 11.
Taarifa hiyo iliendelea kueleza kwamba katika kipindi hicho Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto katika kutekeleza majukumu yake mbalimbali ilitumia Jumla ya shilingi bilioni 46.41 sawa na asilimia 98.71 ya makisio yaliyopangwa kwa mwaka, taarifa ambayo baada ya majadiliano ilipitishwa.
Mbali na taarifa ya Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango, Mkutano huo wa Baraza la Madiwani pia ulipitisha taarifa za Kamati ya Kudhibiti na Kupambana na UKIMWI, taarifa yake iliwasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyoKamati ya Elimu, Afya na Maji, Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira pamoja na Kamati ya Maadili ya Waheshimiwa Madiwani kwa robo ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2023/2024.
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa