- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Lushoto Mh.Methew Mbaruku awaongoza madiwani wote wa Halmashauri kwenye kikao cha baraza kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri tarehe 10/11/2021. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mh. Karist Lazaro, Maafisa Tarafa, wakuu wa Idara mbalimbali wa Halmashauri ya wilaya ya Lushoto, wakiongozwa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Lushoto, Bi.Ikupa Harrison Mwasyoge, Wageni kutoka taasisi mbalimbali za serikali na Binafsi, wawakilishi wa vyama vya siasa, waandishi wa habari na baadhi ya wananchi wa wilaya ya Lushoto.
Katika Kikao hicho Mkuu wa wilaya ya Lushoto, Mh Karist Lazaro alisalimia kwa salamu maaalum ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kazi iendelee.
Mh Karist Lazaro alisisitiza kuhusu ujenzi wa Madarasa ukamilike kwa wakati ili wanafunzi wapate madarasa ya kusomea na kutatua tatizo ilo la madarasa ambayo pesa zimeshatolewa na Rais Samia Suluhu Hassan
Katika Baraza ilo la Madiwani, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Bi.Ikupa Harrison Mwasyoge aliwatambulisha Wataalamu wa vitengo mbalimbali, Wakuu wa Idara Mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Madiwani wote, Wageni wahalikwa na Waandishi wa Habari na kuanza kusoma Ajenda 5 za Mkutano huo wa baraza la Wah. Madiwani wa Tarehe 10/11/2021.
Ajenda hizo zilika ni 1 Kufungua mkutano 2.kusoma na kuthibitisha Muhtasari wa Mkutano wa Tarehe 22/09/2021 3.Taarifa mbalimbali za utekelezaji kwa kipindi cha robo ya kwanza july - septemba.
i. Kamati ya Kuthibiti na Kupambana na UKIMWI.
ii. Kamati ya Elimu, Afya na Maji.
iii.Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
iv. Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
v. Kamati ya Maadili ya Wah. Madiwani
4. Maswala ya Kiutumishi
5.Kufunga Mkutano
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa