- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Lushoto Mh.Methew Mbaruku awaongoza madiwani wote wa Halmashauri kwenye kikao cha baraza kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri tarehe 22/09/2021. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mh .Karist Lazaro ,mwakilishi kutoka ofisi ya RAS Tanga, wakuu wa Idara wakiongozwa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Lushoto, Bi.Ikupa Harrison Mwasyoge, Ma maneja kutoka taasisi mbalimbali za serikali kama vile Tanesco, Luwasa , Mahakama , wawakilishi wa vyama vya siasa pamoja na baadhi ya wananchi wa wilaya ya Lushoto.
Katika Kikao hicho Mkuu wa wilaya ya Lushoto, Mh Karist Lazaro alisalimia kwa salamu maaalum ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kazi iendelee.
Mh Karist Lazaro alisisitiza kuhusu ushirikiano wa Wabunge wote wa Majimbo ya Wilaya ya Lushoto, Afisa tarafa, Watendaji wa Kata, Watendaji wa Vijiji, Wenyeviti wa vijiji na Mitaa ili kurahisisha utendaji kazi.
Pia alitoa pongezi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Lushoto, Bi.Ikupa Harrison Mwasyoge na Kamati ya mitihani kwa namna walivyoshirikiana katika kusimamia mtihani wa darasa la saba ambao ulifanyika kwa siku mbili Tarehe 08/09/2021 na tarehe 09/09/2021 Tanzania.
Mwisho, Mkuu wa wilaya ya Lushoto, Mh. Karist Lazaro alihitimisha kwa kusema kua ataanza Ziara yake ya Wilaya nzima ya Lushoto ya kukagua miradi yote ya Maendeleo na kusikiliza na kutatua Kero za Wananchi wa Wilaya ya Lushoto
Katika Baraza ilo la Madiwani, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Bi.Ikupa Harrison Mwasyoge aliwatambulisha Wataalamu wa vitengo mbalimbali, Wakuu wa Idara Mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Madiwani wote, Wageni wahalikwa na Waandishi wa Habari na kuanza kusoma Ajenda 7 za Mkutano huo wa baraza la Wah. Madiwani wa Tarehe 22/09/2021.
Ajenda hizo zilika ni 1 Kufungua kikao 2.Kiapo cha Diwani Mteule kata ya Gare Mh. Ernest Pascal Sempeho 3.kusoma na kuthibitisha Muhtasari wa mkutano wa Tarehe 29/09/2021. 4. Taarifa mbalimbali za utekelezaji kwa kipindi cha robo ya nne ya Mwezi Aprili - Juni 2021. Taarifa hizo ni
i. Kamati ya Kuthibiti na Kupambana na UKIMWI.
ii. Kamati ya Elimu, Afya na Maji.
iii.Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
iv. Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
v. Kamati ya Maadili ya Wah. Madiwani
5. Kupitia Ratiba ya Vikao kwa Mwaka wa fedha 2021/2022. 6. Maswala ya Kiutumishi 7. Kufunga kikao
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa