- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
Mkutano wa baraza la wah. Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Lushoto umefanyika tarehe 19/11/2019 na kupokea taarifa mbalimbali kutoka katika kamati za kudumu za Halmashauri kwa kipindi cha robo ya nne(aprili -june) 2018/2019. Katika kikao hicho kamati zifuatazo zililiwakilisha taarifa zao kama ifatavyo:-
Katika kikao hicho pia kilihudhuliwa na Kamati ya ulinzi na kamati ya Ulinzi na usalama ikiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Lushoto Mh, January Lugangika, Viongozi wa vyama vya siasa vikiongozwa na mwenykiti wa chama tawala Mh, Rashid Karata na katibu wake Mh. Mahanyu. Pia kikao hiki kilihudhuliwa na Msaidizi wa katibu tawala wa mkoa ambaye anashughulika masuala yote ya serikali za mitaa ndg Kazimoto, Wakuu wa Idara na vitengo kwa ajili ya kutoa ufafanuzi kwa baadhi ya hoja zilizoibuliwa na madiwani
Katika kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Lucas Shemdolwa aliwakaribisha viongozi wa chama na serikali kutoa salamu zao mabalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Lushoto. Katika salamu zake Mh.Mkuu wa Wilaya kwanza alitoa pole kwa wilaya zilizopata maafa ya mafuriko hasa hasa wilaya ya Handeni na Korogwe ,Mapokezi ya fedha kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya barabara iliyoharibiwa na mvua , Hali ya chakula katika Halmashauri ya Lushoto na bei ilekezi. Pia aliwapogeza wenyeviti wa vijiji na vitogonji waliopita bila kupingwa katika uchaguzi wa serikaliza mitaa unaoendelea hii inatokana na usimamizi na mafanikiwa ambayo nchi inayoyapata kutoka na uongozi thabiti wa Rais wa awamu ya tano Mh.Dk John Pombe Magufuli.Pamoja na mafanikio hayo Mkuu wa wilaya ya Lushoto aliwahimiza watendaji wa vijiji kusoma mapato na matumizi katika vijiji vyao na watendaji ambao hawajafanya hivyo kufanya hivyo kabla ya tarehe 2/12/2019.Pia mkuu huyo wa wilaya alisisitiza semina kwa viongozi wapya ili waweze kujua wajibu wao na mipaka yao ya kazi.
Kuhusu kuhifadhi hifadhi za mazingira mkuu huyu wa wilaya alitoa taarifa ya uwepo wa miti ya kutosha kwa ajili ya kupanda maeneo ambayo yako wazi ili kurudishia uota wa asili na kuhimiza kila mtendaji hahakishe anapanda miti takribani miti 455,000 katika kata yake amabayo tayari ameishaiandaa kwa kushirikiana na wadau wa mazingira wa (friends of Usambara) kazi ni kwenda kuichukua na kuipanda katika maeneo husika.
Kuhusu mikopo kwa wanawake ,vijana na watu wenye ulemavu mkuu wa wilaya aliiangiza Halmashuri kutoa mikopo hiyo kwa kila robo ilikuepuka usumbufu kwa kipindi cha mwisho wa mwaka
Katika Kikao hicho wenyeviti wa kamati waliwasilisha taarifa zao kisha wajumbe walitoa michango na maswali yao amabayo yalijibiwa na wenyeviti wa kamati wakisaidiwa na wakuu wa idara husika.Katika kamati ya kupambana na na kudhibiti ukimwi wajumbe walipewa taarifa ya utekelezaji wa shughuli yakutoa mafunzo ya kuwaelemisha juu ya jamii kujua afya zao mapema kwa kupima n, wajumbe walioji ni watugani walipima na kugundilika wameadhirika.Katika majibu ya swali hilo wajumbe walielezwa na mwenyekiti wa kamat kwamba elimu inayotolewa ni kuwashawishi watu kupima kwa hiari na majibu ni swali la mtu binafsi na halazimishwi kutangaza.Katika kamati ya Elimu Afya na Maji wajumbe walioji upungufu wa dawa katika hospitali ya wilaya pamoja na watu kuwa na bima ambalo swala hilo mganga mkuu alilitolea ufafanuzi mzuri kuwa dawa zote muhimu (tracer medicine) zipo za kutosha labda zile zamahitaji maalum.Kuhusu mradi wa maji shume kukwama licha ya miundombinu kukamilika kwa asilimia karibu 80% injinia wa maji alilitolewa ufafanuzi vizuri tatizo lililokwamisha mradi huo la kodi limeishatatuliwa na mkandarasi yuko mbio kupeleka vifaa hivyo site kumalizia kazi hiyo . Kikao hicho kilimalizizika baada ya wajumbe kuridhika na ufafanuzi wa wenyeviti wa kamati na kupitisha taarifa hizo.
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa