- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh.Adamu Malima aongoza kikao maalum cha Baraza la Halmashauri ya wilaya ya Lushoto la kujibu hoja za mkaguzi wa nje(CAG) kwa mwaka wa fedha 2019/2021 pamoja na maagizo ya kamati ya bunge LAAC. Katika kikao hicho Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri Bi . Ikupa Harrison Mwasyoge wakati anatoa taarifa fupi ya ukaguzi ulifanywa na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020 , Halmashauri ya wilaya ya Lushoto ilikaguliwa na kupata HATI SAFI katika ukaguzi wa jumla na ukaguzi wa mradi wa mfuko wa pamoja wa afya unaojulikana kama (Health Basketi Fund.).Pia katika kikao hicho Mkurugenzi mtendaji alitoa taarifa ya Hali halisi ya Hati katika matumizi ya fedha za serikali kwa miaka mitatu mfululizo ambayo imeonyesha Halmashauri ya Lushoto ilikuwa ikifanya vizuri kwa miaka yote mitatu mfululizo kwa kupata HATI SAFI.
Katika taarifa Mkurugenzi mtendaji alibanisha kuwa mpaka sasa hoja za nyuma zimebaki 30 kwa hoja za jumla na hoja 10 kwa mradi wa mfuko wa pamoja wa afya unaojulika na kwa lugha ya kigeni (Health Basket Fund), na hoja za mwaka wa fedha wa 2019/2020 zikiwa zimebaki 45 katika ukaguzi wa jumla na hoja 5 katika mfuko wapamoja wa afya( Health basket Fundi) pamoja na maagizo ya kamati ya Bunge ya hesabu za serikali ya mitaa(LAAC) ambazo zimeletwa katika kikao hicho ili zijadiliwe na kutolewa maoni yake na waheshimiwa madiwani.
Katika kikao hicho Mh Mkuu wa Mkoa alisisitiza uwajibikaji wa kila Mtaalamu katika kila sekta na mgawanyo wa madaraka,kilimo chenye tija kwa wananchi(smart agriculture) .umuhimu wa kutunza mazingira ,utalii wa asili na kupiga marufuku uhamisho wa walimu husio na tija kwa kisingizio cha ugonjwa na baridi.
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa