- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
Mkuwa mkoa wa Tanga afanya ziara fupi ya kujitambulisha rasmi katika wilaya ya Lushoto na kufanya kikao kifupi na kamati ya fedha na Mipango wakiwawakilisha wah. madiwani, wakuu wa Idara Halmashuri ya lushoto wakiwawakilisha watumishi wa Halmashauri pia na viongozi mbalimbali wa chama na serikali katika Halmashauri ya Lushoto. Katika ziara hiyo aliongozana na kamati za ulinzi na Usalama za Mkoa na wilaya zikiongzwa na mkuu wa Wiaya ya Lushoto na baadhi ya watumishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa kiongozwa na katibu Tawala wa Mkoa na katibu Tawala wa wilaya ya Lushoto akiwa na mwongozaji wa kikao hicho(MC) . Katika kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi Ikupa Harrison Mwasyoge alimsomea taarifa ya utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya katika idara mbalimbali za Halmashauri mafanikio na chagamoto ambazo Halmashauri inaendelea kuzitafutia ufumbuzi. Hali halisi ya mapato kwa mwaka wa fedha 2022/23 kufikia Mei ambayo inaonyesha Halmashauri imefika asilimia 70% makusanyo ikilinganishwa na makadirio yake iliyojiwekea. Mkuu wa mkoa akijibu taarfa hiyo alisema Halmashauri haina budi kuongeza jitihada za kukusanya mapato ili kufikisha malengo kwa asilimia iliyopo na kipindi kilichobaki cha mwaka wa fedha Halmashauri iko nyuma kidogo. Akisisitiza hilo Mn.Mkuu wa Mkoa alisema kunamaagizo ambayo amewapa Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Halmashuri kama ushauri kama watazingatia maagizo na ushauri aliyowapa wataongeza mapato ya Halmashauri kwa kiwango kikubwa na kutimiza malengo.Pia alisisitiza swala la upendo kati ya viongozi na viongozi na watumishi wanaowaongoza bila upendo hakuna kitu kitakachofanyika mpaka aliutelea mfano ambao bwana wetu yesu kristo alipoulizwa na wanafunzi wake kuwa amri kuliko zote ni ipi yesu alisema ni upendo, hivyo akautolea mfano kwa mtume muhamad ambaye naye alisitiza upendi katika wafuasi wake. Pia alihimiza kufanya kazi kwa bidii ili kuinua uchumi wa kila mtu na Halmashuri nzima na kushuri kilimo cha ngano nacho kipewe kipawa mbele kwa kuwa kutokuweko na mahitaji makubwa ya ngano siku za usoni kutoka na vita inayoendelelea kati ya Urusi na ukraini. Pia alishukuru sana kwa kutunza mazigira hali ya hewa ya lushoto ameipenda sana mpaka anawashagaa watu ambao wanataka kuhama Lushoto kwenda sehemunyingine wasifanye hivyo.hata na mwenyewe alitamani kukaa Lushoto.
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa