- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
MKUU wa Wilaya ya Lushoto, Mhe. Japhari Kubecha amefanya ziara ya utatuzi wa Kero katika Kata ya Manolo, Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto na kufanya kikao cha ndani na viongozi wa chama na serikali, kisha kukagua miradi kadhaa ya maendeleo kabla ya kufanya mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mlifu ndani ya Kata hiyo akiwa na Lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Akiwa Manolo, ambako aliongozana na Kamati ya Usalama ya Wilaya, Wataalamu wa Halmashauri sambamba na wakuu wa taasisi nyingine za umma ndani ya Wilaya ya Lushoto, Mhe. Kubecha alitembelea na kukagua mradi ujenzi wa vyumba saba vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Manolo mradi wenye thamani ya shilingi milioni 196, kabla ya kutembelea mradi wa ujenzi wa jengo la upasuaji katika Zahanati ya Manolo, mradi wenye thamani ya shilingi milioni 36 ambao unatekelezwa na nguvu za wananchi.
Kisha Mhe. Kubecha alitembelea Shule ya Msingi Mwendala iliyopo katika Kijiji cha Madala na kufanya ukaguzi kwenye mradi wa umaliziaji wa chumba kimoja cha darasa ambao una thamani ya shilingi Milioni 12.5 fedha za mapato ya ndani, ambapo alitoa ahadi ya kuchangia mifuko 10 ya simenti ili kufanikisha ujenzi wa boma lingine la darasa katika shule hiyo.
Baada ya hapo, Mhe. Kubecha alifanya Mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mlifu, ambapo alitoa fursa kwa wananchi kuwasilisha kero zao ambapo alizitafutia ufumbuzi kwenye mkutano huo kitendo ambacho kiliwafurahisha wananchi waliofika katika mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi wa chama na Serikali.
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa