- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
Mkuu wa wilaya ya lushoto, Mh. Karist Lazaro akiendelea na ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa wilaya ya Lushoto. Jana tarehe 04/10/2021 alitembelea kata ya Kwai. Katika ziara hiyo, Mh. Karist Lazaro aliongozana na Mbunge wa jimbo la Lushoto, Mh. Shaban Shekilindi, Diwani wa Kata ya Kwai, Mh. Idd Omary, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Lushoto, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Bi. Ikupa Harrison Mwasyoge, Wakuu wa Idara mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto na Wakuu wa Idara wa Taasisi Mbalimbali.
Baadhi ya miradi iliyokaguliwa alianza Kijiji cha Kwai kilichopo Kata ya Kwai kwa kukagua Majengo Mawili ya vyumba vya Madarasa na jengo moja la Nyumba ya walimu katika shule ya Msingi Dindira ambapo aliongozwa na Mtendaji wa kata ya Kwai, Johari Jonas Ndosi na Diwani wa Kata ya Kwai Mh. Idd Omary. Na pia alienda kukagua jengo la Zahanati ya kijiji cha Kwai ambalo limejengwa kwa nguvu za Wananchi.
Mara baada ya hapo alienda katika kijiji cha Kireti kukagua jengo moja la darasa moja katika shule ya Msingi Kireti na pia alienda shule ya Sekondari Kireti kukagua Majengo ya Maabara
Mwisho alielekea kwenye Kijiji cha Kwemakame ambapo alianza kwa kukagua jengo moja la Madarasa mawili Katika Shule ya Msingi Kwemakame na pia alienda kukagua jengo la Zahanati ya Kijiji cha Kwemakame. Mh. Karist Lazaro alipendekeza Zahanati iyo mara itakapokamilika ipandishwe kutoka Zahanati na iwe Kituo cha Afya cha kijiji cha Kwemakame.
Baada ya Ziara iyo ya ukaguzi Mh. Karist Lazaro aliongea na Wananchi katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kwemakami ili kusikiliza kero za wananchi wa Kata ya Kwai. alisikiliza kero za wananchi na kutatua kero mbalimbali zilizopo katika kata iyo ya Kwai. wananchi waliuliza Maswali ya apo kwa apo na kujibiwa na pia kutoa kero zao kwa Mh.Karist Lazaro
Katika kuhitimisha Mkutano uo, Mh. Karist Lazaro alisema viongozi wanatakiwa kutohukumu ila wanatakiwa kutoa usuruhishi. Mwisho alisisitiza ushirikiano wa viongozi katika utendaji kazi na alitoa mfano kwa kusema ushirikiano ni Kama Timu ya Mpira ambayo ujengwa na wachezaji Zaidi ya mmoja na ili timu iyo ifanye vizuri inaitaji ushirikiano wa wachezaji wote.
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa