- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Lushoto, Mhe. Ally Daffa amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Ndg, Ikupa H. Mwasyoge kwa usimamizi bora wa miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa ndani ya Halmashauri hiyo.
Akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto iliyofanywa na Kamati ya Siasa ya CCM, Mhe. Daffa alisema kwamba ameridhishwa na hali iliyopo katika utekelezaji wa miradi na kumpongeza, Mkurugenzi pamoja na timu yake ya wataalamu kwa usimamizi bora wa miradi.
"Na mimi niungane na wengine (wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Lushoto) na timu yako ya wataalamu kwa usimamizi mzuri, tumepita kwenye miradi na kuona kazi iliyofanyika." Alisema Mhe. Daffa.
Akiwa na Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Lushoto, Mhe. Daffa amefanya ziara na kukagua miradi kwenye Kata za Makanya, Mlalo na Lushoto lengo likiwa kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto
Katika ziara hiyo, Kamati Siasa ya CCM, ilitembelea mradi wa Ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Bombo (M). iliyopo katika Kijiji cha Bombo (M), Kata ya Makanya, Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto wenye thamani ya shilingi milioni 584.2 pamoja na umaliziaji wa Zahanati ya Kijiji hicho wenye thamani ya Shilingi milioni 50.
Baada ya kutoka Kata ya Makanya, ziara hiyo ilitembelea Kata ya Mlalo na kukagua ujenzi wa kinawia mikono, shimo la kondo la nyuma, choo na sehemu ya kuweka tanki la maji katika Kituo cha Afya Mlalo, mradi uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 44 kisha wakakagua ujenzi kituo cha Polisi Mlalo na kumalizia na barabara ya lami inayojengwa kwenye kata hiyo.
Ziara hiyo ya Kamati y Siasa iliishia kwenye Kata ya Lushoto katika Hospitali ya Wilaya ambako ilienda kukagua zoezi la kusimika mitambo ya kuzalisha hewa ya oksijeni ambayo itasaidia wagonjwa Lushoto na Wilaya Jirani.
Katika hatua nyingine: Mhe. Daffa amewataka viongozi wa CCM, kuanzia ngazi ya tawi na kata kuhakikisha wanapita mara kwa mara na kukagua utekelezaji wa miradi kwenye maeneo yao ili kama kuna changamoto taarifa itolewe mapema na itatuliwe, lakini pia ametoa wito kwa wataalamu kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa viongozi wa chama kwenye maeneo yao na si kusubiri hadi uongozi wa Wilaya ufike.
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa