- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
UFAULU wa jumla wa watahiniwa wa darasa la saba kwa mwaka 2023 katika Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto (Lushoto DC) umepanda kwa asilimia 3.66 na kufikia asilimia 58.97, kutoka asilimia 55.31 ya ufaulu wa mwaka 2022.
Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya tathmini ya ufaulu iliyoandaliwa na Afisa Elimu ya Awali na Msingi, Mwl. Eliud Njogellah, ambapo katika taarifa hiyo imeelezwa kwamba kwa miaka minne mfululizo ufaulu katika Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto umekuwa ukipanda kwa kasi kubwa.
Inaelezwa kwamba mwaka 2020, ufaulu wa darasa la saba ulikuwa sawa na asilimia 38.36, mwaka 2021 ukapanda na kufikia asilimia 48.9, wakati mwaka 2022 asilimia 55.31 na mwaka huu ufaulu umefikia asilimia 58.97.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo mwaka 2023, jumla ya wanafunzi 10,938 kutoka katika shule 169 walifanya mtihani na kati ya hao, wavulana 4852 na wasichana 6086, huku waliofaulu wakiwa wanafunzi 6450, wanaume 2786 na wanawake 3664.
Baada ya kupata matokeo haya tayari Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto imeanza kuandaa mikakati ya kuboresha zaidi ufaulu wa darasa la saba mwaka 2024, ambapo juzi, Maafisa Elimu Kata na Walimu wa Kuu wa Shule zote za Serikali walikutana na Kamati ya Uongozi, Fedha na Mipango ya Halmashauri ili kujipanga kufanya vizuri zaidi mwakani.
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa