- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
Mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya wilaya ya lushoto umefanyika leo tarehe 11/12/2020 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri, Mkutano huo ulifunguliwa na Ndg.Nicodemus Tambo Katibu Tawala(W) na kuwapongeza Wah.madiwani kwa kuchaguliwa na kuwataka wakawatumikie wananchi katika maeneo yao.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri(W) Bi. Ikupa Harrison Mwasyoge alisoma agenda nane za mkutano huo ambazo ni kufungua kikao,Uapisho wa Wah.Madiwani,Kiapo cha maadili kwa wah.Madiwani,Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri na makamu mwenyekiti wa halmashauri,Kuunda kamati za kudumu za halmashauri na kuchagua wenyeviti wa kamati,Kupitisha na kujadili ratiba ya vikao vya halmashauri na kamati za kudumu,Kupokea taarifa ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri kipindi ambacho Baraza la madiwani lilivunjwa na agenda ya mwisho nikufunga mkutano.
Katika mkutano huo Mh.Methew Paulo Mbaruku-Diwani kata ya Magamba alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Lushoto kwa kupata kura 45 kati ya 45 zilizopigwa ambayo ni sawa na 100%,pia Mh.Hatibu Zuberi Ulanga-Diwani kata ya Mbaramo alichaguliwa kuwa Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Lushoto ambae alipata kura 44 kati ya 45 zilizopigwa sawa na 97%.
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa