- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Lushoto Mh. Kalist Lazaro leo tarehe 6/8/2021 amezindua rasmi zoezi la chanjo ya covid -19 kiwilaya katika hospitali ya wilaya ya Lushoto. Katika uzinduzi huo ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama, viongozi wa dini na baadhi ya viongozi waandamizi katika wilaya ya lushoto , wakuu wa Idara wakiongozwa na wakurugenzi wa Halmashauri zote mbili Lushoto na Bumbuli.Katika uzinduzi huo Mh.Mkuu wa wilaya ameseme mwenyewe yuko tayari kuchanjwa yeye na familia yake ndiyo maana amekuja nayo, hana mashaka yoyote na chanjo hiyo ya Johnson &Johnson ambayo imezinduliwa hivi karibu na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan.Katika zoezi hilo la utoaji wa chanjo alivitaja vituo ambavyo vitahusika na zoezi hilo katika walaya nzima ya lushoto kutakuwa na vituo sita kwa Halmashauri ya Lushoto kutakuwa na vituo vitatu ambavyo ni Hospitali ya wilaya ya lushoto,kituo cha afya cha Mlalo,pamoja na Mnazi. Katika Halmashuri ya Bumbuli nako kutakuwa na vituo vitatu ambavyo ni Hospitali inayomilikiwa na KKKT , kituo cha afya soni na Mgwashi.
Katika uzinduzi ho kaimu mganga mkuu Dr Ghasto stephano alimueza Mkuu wa wilaya kuwa Halmashuri ya Lushoto imepokea chanjo 2400 na pia ametoa hali halisi ya maambukizi ya ugonjwa huo katika Halmashuri ya Lushoto kuwa yapo kwa kiwango fulani kutokana na sampuli zinazotumwa mkoani kuonekana zinamaambukizi ya corona.Pamoja na maambukizi hayo katika Halmshauri ya Lushoto kaimu mganga mkuu aliwatoa hofu wananchi juu ya chanjo ya Johnson&Johnson kuwa ni bora na haina madhara yoyote kwa hiyo ni muhimu kupata chanjo hiyo dhidi ya ugonjwa wa covid-19 kwa kuanzia kwa makundi ambayo yako katika mstari wa mbele na yale makundi maalum yaliyoanishwa na wizara ya afya.
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa