- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
Team ya mpira wa miguu ya Watumishi Lushoto District Council watawakilisha mkoa wa Tanga kwenye mashindano ya Azam Federation (FA) nafasi hiyo imepatikana baada ya Team ya Watumishi LDC kuibuka washindi kwenye mchezo kati ya Watumishi LDC na Makorora Stars kwenye mchezo uliochezwa leo tarehe 10/11/2021 katika uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Team ya Watumishi LDC wakiongozwa na kocha wao Godfrey Mseli na Afisa Michezo wa Halmashauri ya wilaya ya Lushoto Keneth Mapongo ambaye ndiyo Team Meneja walilazimika kusafiri kutoka Wilayani Lushoto mpaka Tanga jiji kwaajili ya Mchezo huo, wakiwa Wilayani Lushoto. Team hiyo ilifika Katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, wakiwa Ofisini hapo waliagwa rasmi na Wakuu mbalimbali wa Idara. Wakuu hao wa Idara waliongozwa na Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Lushoto Bi, Ikupa Harrison Mwasyoge
Mchezo huo ulianza mnamo majira ya saa 10:00 kamili jioni ambao ulichezeshwa na refarii Ally Ramadhan na waamuzi wasaidizi Sadiki Bakari na Antony Kimbasha na mwamuzi wanne akiwa ni Asha Ally.
Kikosi cha kwanza cha watumishi LDC kilikua na wachezaji Gerald Mwasa, Sijari Salimu, Saidi Hatibu, Ally Yalinda, Julius Kabunda, Ibrahimu Ramadhan, Christopher Edward, Abdalah Jaha, Maliki Miraji, Hamisi Omary na Florentine Mloka kwa wachezaji wa Akiba walikua ni Frank Sembo, Godfrey John ambaye aliingia dakika ya 46 kwa kuchukua nafasi ya Maliki Miraji, Hamza Bakari, Joseph Mashimba, Khalidi Juma, Karimu Joamkini, Sakadodo Sakadodo ambaye aliingia dakika ya 46 kwa kuchukua nafasi ya Florentine Mloka, Apesi Madambo ambaye alichukua nafasi ya Abdalah Jaha
Katika mchezo uo uliokua mzuri na wakuvutia Mpaka kipindi cha kwanza cha dakika 45 za kwanza kinamalizika team hizo zilikwenda mapumziko zikiwa hazijafungana kipindi cha pili kilianza huku team zote zikishambuliana. Katika dakika ya 73 ya mchezo huo mshambuliaji Hamisi Omary aliifungia Team yake ya Watumishi LDC bao pekee na la ushindi, Mpaka filimbi ya Mwisho ikipulizwa na refarii Ally Ramadhan, Makorora stars 0 – 1 Watumishi LDC.
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa