- mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezajia
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha habari
Jana tarehe 27/09/2021. Mkuu wa wilaya ya Lushoto, Mh. Karist Lazaro alifanya ziara ya kukagua Miradi ya maendeleo na Kusikiliza na kutatua Kero za Wananchi wa Wilaya ya Lushoto, akianza na Kata ya Lushoto. katika ziara iyo Mh. karist Lazaro aliongozana na Mbunge wa jimbo la Lushoto Mh. Shaban Shekilindi, Diwani wa Kata ya Lushoto Mh. Moka Urban, Wah. Madiwani wa viti Maalum wa Tarafa ya Lushoto, Viongozi wa chama Cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya lushoto, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto na Wakuu wa Idara mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.
Baadhi ya miradi iliyokaguliwa ni Shule ya sekondori Shambalai, Shule ya Msingi Mbula B, Soko kuu na Jengo la Mama na Mtoto la Hospital ya wilaya ya lushoto, baada ya kukagua miradi hiyo ya Maendeleo, Mkuu wa wilaya ya Lushoto Mh.Karist Lazaro alikutana na Wananchi katika eneo la Lushoto-sokoni. Wananchi wa Kata ya Lushoto walipata wasaa wakutoa kero zao Kwa Mh Karist Lazaro. Na mara baada ya mkutano huo kumalizika wananchi wa Kata ya Lushoto walipa nafasi ya kupata chanjo ya Uviko-19 (Covid-19) ambayo ilitolewa bure kwa Wananchi ambao walikua na utayari wa kupata chanjo hiyo.
MAGUZONI, 18 BARABARA YA HALMASHAURI, 21782 Lushoto,Tanga
Postal Address: P.O.BOX 32 Lushoto
Telephone: +255(027)2977216
Mobile: +255 755 723 374
Email: ded@lushotodc.go.tz
Hatimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.Haki zote zimeifadhiwa